Utangulizi

Juhudi Cooperative and Credit Society  
(Juhudi Saccos) ni ushirika wa akiba na mikopo unaoundwa na wakazi wa Mzinga- Kibeberu na wakazi wa maeneo ya jirani ya jijini Dar es Salaam.
Ushirika huu umesajiliwa mnamo tarehe 20 ya mwezi wa kwanza mwaka 2014 kama asasi ya kutoa huduma za kifedha chini ya sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2014.

Dira.
Kukuza chama chenye uwezo wa kujiendesha kwa kulipia gharama zake, kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha ya wanachama bila ya kutegemea Asasi/ Mamlaka/Watu wengine na kutoa msukumo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuwa sehemu ya mtandao wa huduma za kifedha katika misingi, njia na taratibu za ushirika.

Chama kitaongozwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Misingi ya Ushirika. Misingi hii ni mwongozo ambao vyama vya ushirika hutekeleza kwa vitendo. Chama kinawajibika kuheshimu misingi saba ya ushirika ya kimataifa kama ifuatavyo:-

  • Uanachama uliowazi na wa hiari
  • Udhibiti na utawala wa wanachama kidemokrasia
  • Wanachama kushiriki kiuchumi
  • Uhuru na kujitawala
  • Elimu, mafunzo na taarifa
  • Ushirikiano miongoni mwa vyama vya ushirika
  • Kujali na kujihusisha na jamii 

Mashamba ya mbogamboga ya wakulima wadogo















​Dhima.
​Kukusanya akiba na amana kwa ajili ya kuwakopesha wanachama kwa riba na masharti nafuu na kuwaelimisha namna ya kutumia mikopo hiyo kwa busara ili kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuchumi na maisha bora.


Malengo yetu kwa mwaka 2014-2016.
​Kusaidiana, kustawisha na kuwezeshana katika shughuli za ujenzi wa taifa kwa kufuata taratibu na misingi ya ushirika, na ili kuyafikia haya yote ushirika huu utafanya mambo yafuatayo:-.

  • Kushawishi watu ambao sio wanachama kujiunga na umoja ushirika huu
  • Kupokea hisa, akiba na amana toka kwa wanachama
  • Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanachama
  • Kupambana na ujinga, umasikini, maradhi na ubaguzi hasa wa kijinsia 
  • Kuhifadhi katika mashirika ya fedha na kununua dhamana za serekali baada ya kutoa huduma ya akiba na mikopo kwa wanachama
  • Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote za kiuchumi kwa manufaa ya wanachama kama itakavyokubaliwa katika mkutano mkuu
  • Kujenga ushirika wenye wenye uwezo wa kujiendesha wenyewe na kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wanachama wake na kuchochea msukumo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pia kuwa sehemu ya mtandao wa kifedha katika misingi na taratibu za ushirikiano  nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment